POLITICAL ANIMALS IIIC.

01. 

Kuna muda huwa tunajitafutia matatizo sisi wenyewe kwa kuunda urafiki na watu ambao tulitakiwa tuwasalimie tuu na kuwapita ๐Ÿ˜’. Na @njamasi


02.

Unapoenda kwenye ofisi za watu hakikisha unamsalimia kwa heshima mlinzi au wale wanao fanya usafi mule ofisini, baraka zipo kila mahali ๐Ÿ™. @njamasi

03.

Kamwe Usijutie Siku Katika Maisha Yako. Siku Nzuri Zinakupa Furaha, Siku Mbaya Zinakupa Uzoefu, Siku Mbaya Zaidi Zinakufunza Na Siku Nzuri Zaidi Zinaweka Kumbukumbu. Muwe Na Siku Njema. @lady_bahati

04.

Leo ni kesho uliyoisema jana. Usisite kufanya utakachoona ni bora kwa upande wako, siku zote kubali makosa lakini kamwe usijutie maamuzi yako.Maamuzi yako ni bora na ya msingi kuliko majuto.๐Ÿ‘‰@georgenyakita

Mzingasiasah.blogspot.com

05.

 Mtu umenipa namba yako vizuri tu, nakutext unaniita broo! Kwani nimekwambia natafuta ndugu zangu waliopotea๐Ÿคจ๐Ÿšฎ๐Ÿšฎ 

06. 

Sema wanawake ni wavumilivu sana ila wakichoka kuvumilia ni vita nyingine hata shetan mwenyewe huwa anaweka pozi kwa kiti achukue ujuzi ๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚@julius_MZA

07.

Upendo sio kitu bila vitendo. Kua miniana sio kitu bila uthibitisho. Na pole sio kitu bila mabadiliko;๐Ÿ‘‚@dismasmaliza

08.

Kama hupendi Wali Maharage ni muda muafaka uondoke utuachie nchi yetu. @marekamalili

09

Katika maisha lazima uwe na watu waliokuwa kinyume na wewe, watu wenye wivu juu ya mafanikio yako, watu wanao kukosoa ingali umefanya jambo jema, wakubali watu hao wachukulie kama changamoto katika mafanikio yako ili uzidi kupambana zaidi✍️@nyiwhili

10.

Haijarishi ni mara ngapi nyoka hujivua gamba lake, atabaki kuwa nyoka tu, kwahiyo kuwa makini pindi utakapo waruhusu tena watu warudi katika maisha yako.@bhailee19

11.

Acha kuwaruhusu watu ambao hawatambui thamani yako, wachukue jukumu kubwa katika maisha yako na waingilie ukuu wako.ACHA; @moowzey21

12.

Katika maisha tunatokea katika mazingira magumu sana,

Tumebeba historia nzito za maisha yetu mabegani mwetu, 

Tunapambana kujikwamua,

Ikitokea tumefanikiwa basi usituchukie, wala usituwekee vikwazo mbele yetu maana nyuma yetu kuna kundi kubwa la watu wanaotutegemea, ukituharibia sisi basi utakuwa umeumiza wengi mno. 

Ukishindwa kutushika mkono basi tuache tujifie wenyewe mbele ya safari, lakini usikae mbele yetu ili kutuwekea ukuta kwani utawakomesha wasio na hatia walio nyuma yetu.@safarimlevi

13.

Wape ruhusa watengeneze mipaka wenyewe katika maisha yao, ili utakapoishi kutokana na mipaka yao wasije kusema unajitenga.@mwana_liverpool

14.

Sio kila mtu anastahili katika maisha yako ukiona mtu anatka kuondoka muache aende hata majani kuna wakt upukutisha majani yake ili kuruhus majani mengne kuota. @boazstephen.

15.

Usimdharau Sana mtu ambae anakujali kisa tu huna hisia juu yake, ipo siku utamsukuma na ataondoka hatorudi Tena halafu ukaja kumuhitaji kipindi ambacho kashakusahau !!!! . Ratipher01

16

Tulipokuwa wadogo tuliandika kwa kutumia penseli, ila sasa ukubwani tunatumia kalamu za wino kuandikia.

                                                    

Je umewahi kujiuliza ni kwa nini ipo hivyo? Basi kumbuka kuwa, makosa ya utotoni ni rahisi kufutika, ila si yale ya ukubwani. Kadri ya unavyozeeka, tenda wema. @Hatib147

17.

Hatupambani ili Kumuonyesha Nani Tuna Nini Maishani bali Tunapambana Ili Kurekebisha Hali Halisi Tuliyoikuta Maishani Mwetu. @Dr_josee10

18. USIFANYE BIASHARA NA NDUGU.

hii ni zaidi ya ukicheka na nyani utavuna mabua


Kalibu upate habali za burudani na siasa kwenye ukurasa pendwa wa mzingasiasah.blogspot.com

Comments

Popular Posts