FEAR WOMEN
SABABU NYINGINE YA KUWAOGOPA WANAWAKE
#UZI (TRUE STORY)
Nina jamaa angu ni mwalimu wa shule ya msingi moja mkoani Mwanza, mwezi wa kwanza mwaka huu aliamua kuvuta jiko dada mmoja muuguzi katika hospital mmoja mkoani humo humo japo hakufunga ndoa ya kanisani.
Maisha baada ya jamaa kuamua kuishi pamoja na ile pisi yakikuwa matamu kwa walipendana sana! baada ya miezi miwili kupita jamaa alianza kuletewa stori kuwa demu wake anachepuka na daktari mmoja hospitali pale, mapenzi ni upofu sometimes kwani jamaa alipuuza hizo taarifa
Siku zikaenda, baada ya muda kidogo boda anaempelekaga manzi wa jamaa akamchana mwana oya si kwa ubaya ila demu wako anaku cheat bro, talk to her! jamaa hakukaza fuvu this time!
Jumapili iliyopita ya tarehe 14 mwez huu demu alitoa taarifa kwa mchizi kuwa jumatatu na j4 ya wiki hiii atakuwa na night shift afu then day off! jamaa akasema poa nitawahi kutoka shule nije tu spend time ya mchana wote! J3 ikafika, mida ya saa 12 jioni wife akaaga anasepa job jamaa akamuaga na kumtakia safari njema!
Wife akasepa mida ya saa moja na nusu akamcheki mwana akamwambia kuwa alifika salama na yupo anaendelea na kazi sema siku hiyo akadai kuwa kuna wagonjwa wengu hivo atakuwa bize sana!
Mida ya saa nne jamaa akaenda kwa wakaanga chips akanunua kiepe yai akakwea pipa mpaka hospital kwa wife, akafika wodi anayofanyia kazi akasema yeye ni boda na ameagizwa chips na muuguzi mmoja akamtaja jina, yule kiongozi wa wodi wa siku ile akamwambia huyo mbona leo hana shift, yuko day off mpigie simu muongee vizuri!!
Jamaa akapigwa na butwaa kwa muda kidogo! muda anatoka nje ya wodi akawa anampigia simu manzi yake ila simu ikawa haipatikani, jamaa akasema isiwe taabu akamcheki boda wa manzi ake akamuuliza kishikaji tu oya home kwa yule daktari unapafahamu boda akasema ndiyo, jamaa akasema nipe location, akapewa akaanza route! mida ya saa tano na nusu akafika getto kwa daktari, ni kama doc alikuwa amemaliza cha kwanza sijui kwani wakati jamaa amefika pale getto alipiga hodi ila sauti ya doc ilisikika kutoka bafuni vile ikisema babe kamsikilize huyo anaegonga usiku huu! demu kufika akasita kufungua mlango kwani ni usiku, akamuuliza nani wewe jamaa akajitambulisha, manzi akabaha.
Akafungua mlango jamaa kumcheki ni babe wake hakuongea mengi akamwambia kavae twende home, demu akasema mi siendi niache we endelea na mishe zako, jamaa akaanza kufosi demu akamwambia nitakuita mwizi niache, jamaa akahisi utani, manzi akaanza kupiga kelele mwizi mwizi mwizi!!!!!!
Daktari akatoka bafuni chapu na taulo lake mara ghafla majirani hao, kama kawa majirani huwa hatuna habari na kisa, wakamvaa mwana! akachezea kichapo heavy, wakati anadundwa jirani mmoja akasema mbona huyu mtu kama namfahamu, si mwalimu flani huyu na huyu mwanamke mbona ni mtu wake! watu waka stop kichapo kwanza, wakamuuliza yule manzi kwani alikuwa analia kwa pembeni, ya kweli haya, demu akasema mi tushaachana zamani ila bado ananisumbua anataka turudiane afu mi simtaki tena na leo kanifata usiku huu kwa mtu wangu..
Watu wakamuuliza kwanini sasa umemuita mwizi aisee na watu wanakaribia kumuua, demu akasema mi nilivyomwona nikamwambia aondoke hakusikia akawa ananifosi turudi kwake kwa kunivuta nikamwambia nitakuita mwizi ili kumtisha hakusikia ndo nikaita mwizi kweli!
Daah watu wakasikitika ikabidi wafanye utaratibu wa kumkimbiza hospitali, mpaka muda huu toka jumatatu jamaa yuko ICU hajajitambua bado kwani kile kichapo alichopata si cha nchi hii
Fear women
Ogopa wanawake Ila uwapende pia
#philosopherking
Comments